MANCHESTER CITY VS MANCHESTER UNITED: MATCH PREVIEW


MANCHESTER CITY VS MANCHESTER UNITED: MATCH PREVIEW

Man City vs Man United

Huu ni moja ya michezo migumu katika Ligi Kuu England ukiwakutanisha mahasimu wawili wa jiji la Manchester, yaani Manchester City na Manchester United, huku timu zote mbili zikihitaji ushindi kwa hali na mali ili kuweza ama kujiweka katika mazingira ya mazuri ya kushiriki UEFA mwakani au kuchukua ubingwa kama itawezekana.

Manchester City wanaingia uwanjani kupambana na bila ya nahodha na beki wao tegemezi Vincent Kompany ambaye atakosekana kwa takriban mwezi mmoja baada ya kuumia katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Dynamo Kiev uliopigwa katika mwa wiki.

City wamefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa ambapo watakutana na wababe wa Ufaransa Paris Saint-Germain, ilhali wakiwa hawafanyi vizuri katika ligi huku wakikabiliwa na ushindani mkubwa kutoka Leicester, Arsenal, Tottenhma bila ya kusahau West Ham.

City kwa sasa wapo nyuma kwa alama 12 dhidi ya vinara Leicester huku wakiwa nyuma ya Tottenham na Arsenal kuwania nafasi ya pili na ya tatu.

Kwa upande wa wapinzani wao, Manchester United, wanapigana kwa kila hali kuhakikisha wanapunguza pengo la pointi dhidi ya timu zilizo nafasi za juu ili kuweka hai matumaini yao ya kumaliza 'top four', hivyo mchezo wa leo kuwa mgumu wa aina yake.

United wamekuwa na wakati mgumu katika ligi huku wakitupwa nje pia katika michuano ya 'Europa League' baada ya kutolewa na Liverpool Alhamisi ya wiki iliyopita.

Taarifa muhimu kwa timu zote mbili

Kwa upande wa Manchester City, katika eneo la ulinzi, mabeki wao Vincent Kompany na mwenzake Nicolas Otamendi hawatakuwepo kwenye mchezo huu kutokana na kuendelea kuuguza majeraha yao.

Kwenye eneo la kiungo, Kevin De Bruyne atakosekana akiendelea kuuguza jeraha la goti linalomkabili, wengine ni Fabian Delph jeraha la kisigino na Samir Nasri (paja)

Kwa upande wa Manchester United, Ander Herrera kuna wasiwasi wa kutojumuishwa katika mcheo huu akisumbuliwa na maumivu ya nyonga.

Ashley Young na Cameron Borthwick-Jackson wanaweza kurejea baada ya kujumuika na wenzao mazoezini jana, Adnan Januzaj na Timothy Fosu-Mensah watakuwepo baada ya kuthibitishwa kupana na timu ya madaktari wa klabu.

Wayne Rooney bado ataendelea kubaki nje akiunguza jeraha la goti, Luke Shaw (mguu) na Will Keane (nyonga) pamoja na beki Phil Jones pia.

Takwimu muhimu

  • Sergio Aguero amefunga magoli saba kwenye michezo saba dhdi ya United
  • Manchester United wameshinda mchezo mmoja tu kati ya nane ya mwisho ya Ligi ambayo wamecheza ugenini (wameshind mmoja, droo tatu na kufungwa minne).
  • City wameshinda michezo yao minne na kufungwa mmoja dhidi ya United katika michezo sita ya mwisho ya ligi waliyokutana
  • Ni wachezaji watano tu ambao wamefunga zaidi kwenye mchezo dhidi ya United katika historia ya Ligi ya England (Ferdinand, Henry, Gerrard na Fowler wakiwa na magoli nane na Allan Shearer magoli 10).
  • Sergio Aguero anahitaji goli moja tu kufikia rekodi ya kuwa mchezaji mwenye idadi kubwa ya magoli dhidi ya mahasimu wa jiji la Manchester na kuwa sawa na Wayne Rooney (magoli 8). Na akifunga kwenye mchezo huu basi Aguero atakuwa ameweza kufanya hivyo ndani ya michezo nane, wakati Rooney ilimchukua michezo 16 kufikisha idadi hiyo ya magoli.
  • Aguero amefunga magoli 11 katika michezo nane ya mwisho ya Ligi aliyocheza kunako dimba la Etihad Stadium.
  • Manuel Pellegrini anaweza kuingia kwenye rekodi ya kuwa kocha wa kwanza wa Manchester City kushinda 'derby' nne za Ligi endapo atashinda mchezo huo. Kocha wa City wa mwisho kufanya hivyo alikuwa ni Joe Mercer mwaka 1970 (alishinda jumla ya 'derby' tano).
  • City wameshinda michezo ya ligi minne na kupoteza mmoja kati ya michezo sita ya mwisho dhidi ya United.
  • Mchezo wa ligi uliopigwa mwezi Oktoba mwaka jana uliisha kwa suluhu.
  • Mara ya mwisho kwa mahasimu hao kukutana katika dimba la Etihad ilikuwa ni Novemba 2, 2014 wakati Sergio Aguero alipoifungia City goli moja na la ushindi kwenye dakika ya 63.
  • United wameshindwa kushinda mchezo wowote kati ya mitano ya mwisho dhidi ya City waliyocheza ugenini.


Comments