Romelu Lukaku amesema hana tatizo lolote ikiwa atapata nafasi nyingine ya kuwa chini ya kocha ya Jose Mourinho ambaye hapo awali walikuwa wote kunako klabu ya Chelsea.
Mshambuliaji huyo raia wa Ubelgiji amekuwa akihusishwa kuondoka Everton, ambako mpaka sasa ameshaweka kambani mabao 25 kwenye michuano yote msimu huu, huku baba yake Roger akisema kuwa mwanaye amekuwa akitakiwa na vilabu vikubwa vya Ulaya zikiwemo Manchester United na Bayern Munich.
Huku Mourinho akitarajiwa kutua Old Trafford mwishoni mwa msimu huu, endapo Lukaku atajiunga na Man United basi atakutana kwa mara nyingine na Mourinho ambaye hapo awali alimuuza Everton kwa ada ya paundi milioni 28 mwaka 2014.
"Baadhi ya watu watasema kuwa nahitaji kumshawishi lakini sidhani kama kuna haja ya kufanya hivyo. Miaka mitatu iliyopita nilikuwa nina miaka 20 na sikuwa tayari kucheza katika timu zenye presha kubwa", Lukaku amesema.
Takwimu za ufungaji za Lukaku msimu huu;
Mechi alizocheza: 39
Magoli: 25
Comments
Post a Comment