Mafanikio ya Leicester yanavyomuongezea siku za kuishi Mgonjwa wa Kansa Aliyeambiwa Angekufa Baada ya Wiki 2


Mafanikio ya Leicester yanavyomuongezea siku za kuishi Mgonjwa wa Kansa Aliyeambiwa Angekufa Baada ya Wiki 2

Shabiki mmoja wa LEICESTER City mwenye ugonjwa wa kansa ambao upo katika hatua ya mwisho amekaririwa akisema ndoto ya kuona timu yake ikichukua ubingwa wa EPL inampa nguvu ya kupambana na kuendelea kuwa hai.

LEICESTER-main_2753141aAussie Tony Skeffington alipewa wiki nne za kuishi na madaktari baada ya kugundulika na ugonjwa huo mnamo mwezi March 2015.

Wakati huo Leicester walikuwa wakipambana kuepuka kushuka daraja kutoka kwenye Premier League. 02_21094000_7baf6f_2753158aLakini sasa kikosi cha Claudio Ranieri — wanapewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa huo wa England.

Na Tony anazidi kupata tumaini la kuendelea kuwa hai, akiamini ataendelea kupumua mpaka atakapoiona timu yake aliyoanza kuishabiki tangu utotoni ikitwaa ubingwa mnamo mwezi May.

Tony, mwenye miaka 51, alizungumza na kusema: "Kuiangalia Leicester kutoka kupambana kushuka daraja msimu uliopita na kuwaangalia sasa wanavyofanya vizuri kumezidi kunisaidia kuniweka hai na kupambana na huu huo wa kansa.

03_21094000_58135e_2753159a"Wakati madaktari waliponiambia nina wiki nne ya kuishi mwaka jana – Leicester walikuwa wakipambana na kufanikiwa – na mimi nilipambana na kuvuka wiki mbili nilizoambiwa na madaktari.

"Ukiwa na jambo zuri linalokupa furaha inakufanya uwe na furaha. Nina imani nitafanikiwa kuishi mpaka mwishoni mwa msimu.

Mkewe aitwaye Donna aliongeza: "Leicester City wanamfanya aendelee kupambana na kuwa hai."

Tony amekuwa na matumaini ya kusafiri kwenda UK kuiangalia timu ya mashujaa wake kabla hajaondoka duniani.

Lakini ugonjwa umemzidi na Tony ambaye anaishi huko Adelaide imebidi aiharishe mipango yake.

 



Comments