MACHESTER UNITED YAITUMBUA MANCHESTER CITY ...nyota ya kinda Marcus Rashford yazidi kung'ara, aweka historia mpya Manchester
Kinda wa miaka 18 na siku 141, Marcus Rashford anakuwa mchezaji kijana zaidi kufunga katika historia ya mechi za watani wa jiji la Manchester - Manchester United na Manchester City.
Akicheza soka la hali ya juu, dakika ya 16 Marcus Rashford akaifungia Manchester United bao pekee liliowapa ushindi wa 1-0 vijana wa Louis van Gaal dhidi ya Manchester City katika mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa Etihad Stadium.
Rashford ambaye hili linakuwa ni bao lake la tano katika mechi nane alizocheza, alipita beki mkongwe Martin Demichelis na kumchambua kipa Joe Hart.
Ushindi huu unaweka hai matumaini ya Manchester United kumaliza kwenye 'top four' huku nafasi ya Manchester City kuwania ubingwa ikiyoyoma kizani.
Manchester United (4-2-3-1): Hart (Caballero 50mins); Sagna, Demichelis (Bony 53), Mangala, Clichy; Toure, Fernandinho; Navas, Silva, Sterling (Fernando 26); Aguero.
Manchester United (4-2-3-1): De Gea; Darmian (Fosu-Mensah 84), Smalling, Blind, Rojo (Valencia 62); Carrick, Schneiderlin; Lingard, Mata (Schweinsteiger 70), Martial; Rashford.
Rashford shujaa mpya wa Manchester United
Rashford sasa ana mabao matano katika mechi nane alizocheza
Sir Alex Ferguson (wa pili kushoto) akiwa uwanjani
Mwenyekiti wa Manchester City' Khaldoon Al Mubarak (kulia) akisalimiana na mtendaji wa Manchester United Ed Woodward
Marouane Fellaini leo aliishia benchi
Rashford akimtungua Joe Hart
Fernandinho, Eliaquim Mangala Raheem Sterling hoi
David de Gea anashangilia bao Rashford
Comments
Post a Comment