LUIS ENRIQUE: BARCA NI TIMU AMBAYO NAIHOFIA KWENYE ROBO FAINALI YA UEFA


LUIS ENRIQUE: BARCA NI TIMU AMBAYO NAIHOFIA KWENYE ROBO FAINALI YA UEFA

Henrique

Kocha wa Barcelona Luis Enrique amesema kwamba, kama kuna timu ambayo angeihofia sana katika Ligi ya Mabingwa Ulaya basi ni Barcelona.

Enrique jana alishuhudia timu yake ikiitupa Arsenal nje ya michuano hiyo kwa mabao 3-1 yaliyofungwa na Messi, Neymar na Suarez huku katika mchezo wa kwanza uliopigwa katika dimba la Emirates wakishinda magoli 2-0.

Kwa sasa Barca itapambana na timu kati ya Bayern Munich, Atletico Madrid, Real Madrid, Paris Saint-Germain, Manchester City, Wolfsburg au Benfica baada ya kufanyika kwa droo itakayochezeshwa kesho Ijumaa.

Bareclona wako katika moto usiopimika baada ya kutopoteza mchezo wowote katika mechi 38 kwenye mashindano yote hadi sasa.

"Timu pekee ambayo nisingependa kukutana nayo ni Barca", Luis Enrique alisema.

"Ni dhahiri kwamba tuna wachezaji wa kipekee, lakini mwisho wa siku kitu kizuri zaidi ni kwamba wachezaji wanacheza kwa ushirikiano mkubwa katika nyakati zote za kushambulia na kulinda".

"Tuna furaha kubwa kwamba Messi, Suarez na Neymar ni washambuliaji wetu" .



Comments