LOUIS VAN GAAL amekiri kwamba wakikubali kipigo nyumbani kwa Manchester City wikiendi hii ndio mwisho wa matumaini ya Manchester United kumaliza Premier League katika timu nne za juu - top four.
Kocha huyo raia wa Uholanzi kwa msimu wote huu alibaki na matumaini kwamba Red Devils wanaweza kufuzu kwa msimu ujao wa Champions League.
Lakini baada ya kutolewa na Liverpool katika Europa League, Van Gaal sasa dalili ya kufeli inaonekana kutanda katika sura yake, na anatambua jinsi gani Manchester derby ilivyo na umuhimu.
Alipoulizwa kama mechi hiyo ni ya kufa au kupona kwa United, alisema: "Nadhani hivyo. Yeah, tuko pointi nne nyuma kwa sasa. Kwa hiyo unatakiwa kushinda vinginevyo pengo ni kubwa na kubwa zaidi, na mechi unazotakiwa kucheza ni chache.
"Basi ni pointi saba na tunatakiwa kucheza mechi nane. Ni ngumu sana kupata auheni kwa pengo hilo. Ni vigumu kwa sababu West Ham United pia iko mbele. Hivyo sit u City, lakini pia West Ham United."
Comments
Post a Comment