LIVERPOOL imeripotiwa kumuweka katika orodha yake ya uhamisho wa majira ya kiangazi hiki kinda wa Chelsea, Domingos Quina hatua ambayo inaelezwa kuwa itazua hasira kwa mashabiki wa Stamford Bridge wanaomzimia kiungo huyo.
Ripoti zinaeleza kwamba Manchester United walikuwa karibu katika dili la Quina, lakini wapinzani wao wakubwa, Liverpool wameingilia kati kutaka kumaliza biashara na kinda huyo.
Kwa mujibu wa Daily Mail, Liverpool walikuwa jukwaani waki iliyopita wakimtazama staa huyo wa kikosi cha Ureno cha vijana wa chini ya miaka 17 akicheza dhidi ya Croatia na sasa wana nia ya kumpeleka Anfield.
Quina bado hajacheza katika timu ya kwanza ya Chelsea, lakini tayari kipaji chake kinazitoa udenda Arsenal, Tottenham na Manchester City zinazopigana vikumbo kumtoa Stamford Bridge.
Comments
Post a Comment