LIVERPOOL HAWATAISAHAU SOUTHAMPTON ...TOTTENHAM NAYO YAUA, BENITEZ APATA POINTI YA KWANZA NEWCASTLE



Senegalese midfielder Mane (second left) scores his            team's first goal of the game as Mignolet fails to keep out            his strike

Liverpool wamekutana na kipigo ambacho hawatakisahau kutoka kwa Southamtpon katika mchezo mkali wa Premier League.

Kikosi cha Jurgen Klopp kilikuwa kimeushika vilivyo mchezo na kuonekana kama vile kingeibuka na karamu ya magoli lakini mwisho wa siku wakalala 3-2.

Liverpool ilikwenda mapumziko ikiwa mbele 2-0 kwa magoli ya Coutinho na Sturridge 22 yaliyopatikana katika dakika ya 17 na 22.

Lakini mambo yalianza kubadilika kuanzia dakika ya 64 pale mchezaji aliyetokea benchi  Sadio Mane alipoifungia Southampton bao la kwanza, hiyo ikiwa ni baada ya kuanza kwa mkosi wa kukosa penalti dakika ya 50.

Dakika ya 86 Graziano Pelle akatupia wavuni goli la kusawazisha, kabla ya Mane ambaye hapo kufunga tena dakika ya 86.

Southampton: Forster, Martina, van Dijk, Fonte, Bertrand, Steven Davis, Romeu (Ward-Prowse 69), Clasie (Wanyama 45), Tadic (Mane 45), Long, Pelle

Liverpool: Mignolet, Clyne, Lovren (Skrtel 45), Sakho, Flanagan, Lallana, Allen (Ojo 87), Can, Coutinho, Sturridge (Benteke 70), Origi.

Katika michezo mingine, Tottehnam imezidi kujiimarisha katika mbio za kusaka taji la Ligi Kuu baada ya kuifumua AFC Bournemouth 3-0 kwa magoli yaliyofungwa na Harry Kane (mawili) na Christian Eriksen.

Kocha mpya wa Newcastle Rafa Benitez amepata pointi ya kwanza baada ya timu yake kuambulia sare ya 1-1 dhidi ya Sunderland.
Sadio Mane (second from                  left) celebrates with his team-mates after coming off                  the bench to score the winner against Liverpool
Sadio Mane (wa pili kushoto) akishangilia bao lake la ushindi
Mane collected the ball                  after Cuco Martina had won it from Joe Allen and fired                  beyond Simon Mignolet to score in the 86th minute
Mane anaachia mkwaju uliozaa bao la ushindi
Mane's low strike beats                  Mignolet and nestles into the back of Liverpool's net                  for his second goal of the afternoon at St Mary's
Mignolet anaruka bila mafanikio kuzuia mpira wa Mane



Comments