Lini na Wapi Barcelona Wanaweza kutwaa ubingwa wa La Liga


Lini na Wapi Barcelona Wanaweza kutwaa ubingwa wa La Liga

FC Barcelona walimaliza weekend iliyopita kwa kuongeza wigo wa pointi kwenye La Liga baada ya mechi yao na Villareal.

  Sare ya 2-2 katika uwanja wa El Madrigal, dimba ambalo Real Madrid na AtleticoMadrid wote walipoteza michezo yao, iliwafanya Barca kuongeza pointi 1 mbele ya Atletico. Mpaka sasa mahesabu yanaonyesha Barca wanaweza kuanza kujiandaa na maandalizi ya kushangilia ubingwa. 

  Ikitokea kwamba Barcelona na Atletico wote wakashinda mechi zilizobaki – au japo mechi kadhaa zijazo- kikosi cha Luis Enrique kinaweza kushinda ubingwa wao wa 35 katika dimba la Nou Camp katika mechi dhidi ya Sporting Gijon katika mchezo wa 35 wa ligi  (April 23/24). 
Barça kwa sasa wana pointi 76, wakati Atletico wana pointi 67, ingawa rekodi ya head to head inalifanya pengo kuwa pointi 10. Timu hizi pia zitakutana katika robo fainali ya michuano ya Kombe la mabingwa wa ulaya. 

Real Madrid, wakiwa na pointi 66 baada ya ushindi wao dhidi ya Sevilla jumapili, bado wana nafasi finyu ya kuweka hai matumaini yao kwa ushindi katika mechi ijayo dhidi ya Barca pale Nou Camp, mwezi ujao. Wana pointi 10 nyuma ya vinara, lakini wanaweza kulipunguza kufikia pointi 7 huku ikiwa imebaki michezo 7 ligi kuisha. 

  
Michezo mitano ya Barça inayoamua. 

Barça-Real Madrid

R. Sociedad-Barça

 Barça-Valencia

Deportivo-Barça

Barça-Sporting

Ikiwa Barca atashinda mechi hizo zote, watakuwa wamefikisha pointi 91. Ni idadi ya pointi ambazo Atletico hawawezi kufikia. Atletico wakishinda mechi zao zilizobaki watafikisha pointi 82. 

Mechi zao zilizobaki za Atletico 

Atletico-Betis

Espanyol-Atletico

 Atletico-Granada

 Athletic Club-Atletico

Atletico-Rayo V.

Real Madrid pia watashindwa kupata nafasi ya ubingwa ikiwa yatatokea hayo niliyoyaeleza hapo juu. 



Comments