LICHA YA MASHABIKI KUTAKA WENGER AONDOKE, REKODI YAKE NI KUBWA KWA MAKOCHA WA ULAYA


LICHA YA MASHABIKI KUTAKA WENGER AONDOKE, REKODI YAKE NI KUBWA KWA MAKOCHA WA ULAYA

Arsene Wenger

Kituo kinachojulikana kama International Centre for Sports Studies, au CIES kwa kifupi, kimetoa data za makocha mbalimbali kwenye ligi kubwa barani Ulaya ambao wamedumu kwa muda mrefu zaidi kwenye vilabu vyao.

Katika data hizo. Arsene Wenger ndiye kinara kwenye orodha hiyi akiwa kocha aliyedumu kwa muda mrefu zaidi katika klabu ya Arsenal yenye maskani yake Kaskazini mwa jiji la London.

Wakati baadhi ya timu zikiwa na tabia ya kubadilisha makocha kama soksi, Arsenal kwa upande wao, wamekuwa tofauti sana.

Wenger amedumu kwenye klabu ya Arsenal kwa miezi 233.  Baada ya Wenger, kocha wa St Etienne Christophe Galtier ndiye anayefuata kwa karibu zaidi, huku kocha wa Guingamp Jocelyn Gourvennec akishika nafasi ya tatu kwa kudumu klabuni hapo kwa miezi 70 mpaka sasa.

Kwa kuangalia kwa umakini data hizi, mameneka wengi kwa sasa wanadumu kwa kipindi cha mwaka mmoja, hii ni kutokana na uwiano wa takwimu zinavyoonesha.

Angalia data hizi hapa chini



Comments