Barcelona imejikita kileleni mwa La Liga kwa pointi tisa lakini ingeweza kuongoza kwa tofauti ya pointi 11 kama wangelinda uongozi wake wa bao 2-0 dhdi ya Villarreal.
Hadi mapumziko Barça ilikuwa ikiongoza kwa magoli ya Ivan Rakitic na Neymar, lakini kipindi cha pili wenyeji Villarreal wakachomoa kupitia kwa Cedric Bakambu na lile la kujifunga la Jeremy Mathieu.
Hata hivyo wenyeji walilalamikia uamuzi mbovu wa waamuzi ikiwemo penalti iliyozaa bao la Neymar.
Ivan Rakitic (kushoto) na Neymar wafungaji wa magoli ya Barcelona
Neymar akishangilia bao lake la penalti tata
Comments
Post a Comment