Kwanini Johan Cruyff alikuwa akivaa jezi namba 14?


Kwanini Johan Cruyff alikuwa akivaa jezi namba 14?

Johan Cruyff alikuwa akivaa jezi namba 14 ambayo kwa wakati wake ilikuwa namba ya jezi ambayo huvaliwa na wachezaji wa reserves. 

  
Hakuwa anaivaa jezi hiyo katika misimu sita ya mwanzo wa maisha yake ya soka, lakini baadae aliamua kuanza kuvaa jezi namba 14. Ilitokea siku moja mchezaji mwenzie wa Ajax – Gerrie Muhren alishindwa kuipata jezi yake namba 7, matokeo yake Cruyff akaona isiwe taabu akampa mchezaji huyo jezi namba 9 ambayo ndio alikuwa akivaa, baada ya hapo Cruyff akaingia kwenye chumba cha utunzaji vifaa na kuchukua jezi ya kwanza aliyoiona – jezi hiyo ilikuwa na namba 14 mgongoni.  

 Walipoingia dimbani Ajax wakafanikiwa kuifunga PSV 1-0,  October 30, 1970, na Cruyff akaamua kwamba waendelee kuvaa jezi namba zile zile katika mcheo uliofuatia – na kilichofuatia ni historia – jezi namba 14 imekuwa inamuwakilisha.

  Alipokuwa Barcelona ilimbidi avae jezi namba 9 kwa sababu La Liga walikuwa na sheria ya namba za uwanjani ziwe kuanzia 1-11 tu na sio vinginevyo. 
Hata katika kombe la dunia mwaka 1974, wakati namba zilipokuwa zikitokewa kwa kufuata mfumo wa herufi, Cruyff alibahatika kupata jezi namba 14. Mwaka 2007, Ajax walifikia maamuzi kwamba jezi namba 14 haitotumika tena kwa heshima ya Cruyff. 



Comments