KUTANA NA MAKOCHA 4 WA EPL WALIOCHEZA MPIRA ENZI ZA UJANA WAO


KUTANA NA MAKOCHA 4 WA EPL WALIOCHEZA MPIRA ENZI ZA UJANA WAO

Enzi zao 1

Kwenye maisha ya ukocha sio lazima kocha awe amewahi kucheza mpira kwa kiwango fulani ili awe kocha mzuri na kuweza kupata mafanikio, wapo makocha ambao hawajui hata kupiga danadana tano lakini wameweza kufanya vizuri kutokana na mbinu walizozipata darasani.

Lakini pia wapo wale ambao wamewahi kucheza mpira kwa ngazi ya kulipwa na baada ya kutundika daruga wakaingia kwenye fani ya ukocha na kuendelea na maisha ya soka wakiwa nje ya uwanja.

Kutana na makocha wanne wa timu kubwa za Premier League pale England ambao wamewahi kucheza soka enzi za maisha yao ya ujana na baadaye wakahamia kwenye mabenchi ya ufundi na kuendelea kufundisha mchezo wa soka.

4. Arsene Wenger – Arsenal

Enzi zao

Wenger alicheza kama kiungo lakini pia beki kwenye klabu kama FC Duttlenheim, Mutzig, Mulhouse, ASPV Strasbourg, RC Strasbourg kati ya miaka ya 1963-1981.

Alianza kuvutikwa na ukocha tangu akiwa bado kijana mdogo. Mfaransa huyo hakuwa na kasi wakati wa mchezo lakini aliweza kuusoma mchezo haraka sana.

Wenger hakuonekana kama mchezaji hadi alipofika umri wa miaka 20, aliona hiyo ilikuwa ni fursa ya yeye kuongeza mbinu za kiufundi. Alipokuwa mwishoni mwa miaka ya 20 ya umri wake tayari alianza kukifundisha kikosi cha wachezaji wa akiba wa RC Strasbourg pamoja na timu ya vijana. Kwasasa ni miongoni mwa makocha wenye majina makubwa na mafanikio kwenye Premier League.

3. Guus Hiddink – Chelsea

Enzi zao 2

Kocha wa sasa wa muda wa klabu ya Chelsea Guus Hiddink ameshazifundisha timu bora duniani na kufanya vizuri kwenye ngazi ya kimataifa lakini kocha huyu amewahi kuupiga enzi za ujana wake. Amewahi kuvitumikia vilabu kama PSV na De Graafschap (ambapo alitwaa taji la Dutch second division) huko Uholanzi na alitumia muda wake huko America kabla ya kuamua kutundika daruga mwka 198

2. Louis van Gaal – Manchester United

Enzi zao 3

Manager wa Manchester United alikuwa ni nyota wa Ajax enzi za utoto wake, wakati huo Johan Cryuff pamoja na Johan Neeskens walikuwa kwenye kikosi cha kwanza. Japokuwa hakupata mafanikio akiwa katika timu hiyo, kiungo huyo wa zamani aliimkia Ubelgiji kutafuta mafanikio kwenye klabu ya Royal Antwerp kisha baadaye akarejea tena Uholanzi na kujiunga na Rotterdam na AZ kisha kuamua kuingia kwenye taaluma ya ukocha.

1. Jurgen Klopp – Liverpool

Enzi zao 4 

Kocha wa Liverpool anakubalika kwenye jiji la Mainz kwasababu kuu mbili, kuwa kocha bora na mchezaji bora wa klabu yao kuwahi kutokea. Mjerrumani huyo alitumia muda mwingi wa uchezaji wake kwenye klabu ya Mainz, alianza kucheza kama mshambuliaji lakini baadaye akabadilishwa na kuwa beki. Akiwa Mainz alicheza zaidi ya mechi 300 na kufanikiwa kufunga magoli 52.



Comments