KIPA WA BARCELONA ASEMA MESUT OZIL NI KAMA MESSI UWANJANI




KIPA WA BARCELONA ASEMA MESUT OZIL NI KAMA MESSI UWANJANI
After a difficult            start to life at Arsenal,  Ozil has been in superb form this            season, with 18 league assists

KIPA wa Barcelona, Marc-Andre ter Stegen amemwagia sifa kiungo wa Arsenal, Mesut Ozil akisema kuwa staa huyo anayecheza naye katika kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani, anarandana kipaji na Lionel Messi.

"Kama mwanasoka, Ozil ni mchezaji ambaye anaweza kufanya 'vitu visivyofikiriwa' dimbani kama alivyo Messi… Anavutia, na sisi tutakuwa macho kwamba hataweza kuleta madhara kwetu.

"Nimecheza pamoja naye mara mbili au tatu na ni mchezaji muhimu sana kwa timu ya taifa ya Ujerumani na anaweza kufanya mambo ya ajabu," alisema.


Kikosi cha Arsene Wenger kitakuwa Nou Camp Jumatano usiku kwa mechi ya marudiano ya Champions League, hatua ya mtoano ya 16 bora kikihitaji kupiku ushindi wa 2-0 waliopata Barcelona katika mechi ya kwanza iliyopigwa Emirates.


Comments