ALEX IWOBI ameanza maisha mapya ndani ya Arsenal inayopigania ubingwa wa Premier League kwa kuonyesha kiwango cha hali ya juu dhidi ya Everton kiasi cha kuwaaminisha mashabiki wa Gunners kwamba zama za Theo Walcott Emirates zimekwisha.
Kinda huyo wa miaka 19 alianza kwa mara ya kwanza katika mechi ya ligi akiwa na Gunners, lakini alionekana kuwa vizuri na kuiweka Arsenal kuwa mbele kwa mabao 2-0, akifunga bao la aina yake kabla mapumziko.
Wimbi limegeuka dhidi ya Theo Walcott katika wiki za hivi karibuni baada ya kuonyesha kiwango kibovu mara kadhaa na mashabiki wengi wanataka fowadi huyo wa England apigwe bei.
Na baada ya Iwobi kufanya kweli dhidi ya Everton, mashabiki kibao wamedai kuwa wakati wa Walcott katika klabu hiyo umekwisha.
Comments
Post a Comment