Kiungo wa West Ham Dimitri Payet na N'Golo Kante wa Leicester wote walifunga magoli huku wakiadhimisha siku zao za kuzaliwa wakati Ufaransa inaibuka na ushindi wa kwanza kwenye uwanja wa Stade de France tangu kutokea kwa shambulio la kigaidi mwezi November mwaka uliopita.
Kante alifunga bao la kuongoza dakika za mapema kwenye mchezo wake ambao alicheza kwa dakika zote 90 kabla ya Andre-Pierre Gignac kupiga bao la pili.
Alexander Kokorin alijibu mapigo kwa kufunga bao la kusawazisha kwa upande wa Urusi lakini Payet alipiga bao akiwa umbali wa mita 30 kwa mpira wa adhabu ndogo ikiwa ni mpira wake wa kwanza kugusa tangu kuingia uwanjani akitokea benchi.
Baada ya Yuri Zhirkov kufunga goli la pili, Payet alipika goli ambalo lilifungwa na Kingsley Coman dakika za lala salama.
Comments
Post a Comment