YAMETIMIA… Hatimaye ratiba ya robo fainali ya Champions League imetoka huku miamba pekee ya England iliyobaki katika michuano hiyo, Manchester City ikiangukia mikononi mwa Paris Saint-Germain (PSG).
City inacheza kwa mara ya kwanza hatua hiyo, lakini kocha wake, Manuel Pellegrini tayari ameonja ladha yake akiwa na Villarreal na Malaga, na ana matumaini ya kujiandikia historia ya kufuzu nusu fainali kabla ya kumwachia mikoba Pep Guardiola mwisho wa msimu.
Katika ratiba hiyo, Bayern Munich itakwaana na Benfica, Wolfsburg na Real Madrid, huku Atletico Madrid ikipewa Barcelona katika vita ya miamba ya ligi moja.
Comments
Post a Comment