JUVENTUS YANYANG’ANYWA TONGE KINYWANI NA BAYERN MUNICH …Vijana wa Pep Guardiola watinga robo fainali
Juventus imeongoza kwa mabao mawili hadi dakika ya 72 kupitia magoli ya Paul Pobga dakika ya 5 na Juan Cuadrado dakika ya 28, lakini mwisho wa siku wanalala 4-2 dhidi ya Bayern Munich kwenye mchezo mkali wa Champions League.
Bayern wanaonolewa na Pep Guardiola walisawazisha kupitia kwa Robert Lewandowski kunako dakika ya 73 na Thomas Mueller aliyefunga dakika ya 90 na kulazimisha timu hizo kucheza dakika 30 za 'Extra Time'.
Miamba hiyo ya Ujerumani ikatumia vizuri dakika hizo 30 kwa kufunga magoli mawili ya haraka haraka dakika ya 108 na 110 yaliyofungwa na Thiago Alcantara na Kingsley Coman na kujinyakulia tiketi yao ya kwenda robo fainali.
Katika mchezo wa kwanza wiki mbili zilizopita huko Italia, timu hizo zilitoshana nguvu kwa bao 2-2.
Comments
Post a Comment