JUVENTUS WATAMBA KUENDELEA KUBAKI NA PAUL POBGA



JUVENTUS WATAMBA KUENDELEA KUBAKI NA PAUL POBGA

MKURUGENZI Mkuu wa Juventus, Giuseppe Marotta amesema kuwa staa wao anayekuja kwa kasi, Paul Pogba amewataarifu kwamba anatarajia kubaki katika klabu hiyo ya Turin, maarufu kama Old Lady.

Pogba mwenye miaka 23, yupo kwenye mkataba na Juve hadi mwaka 2019, lakini hilo halijalizuia klabu kubwa za Ulaya, zikiwamo Paris Saint-Germain, Manchester City na Barcelona kumfuatilia.

Juventus ipo katikati ya harakati za kutetea mataji yao ya Serie A na Coppa Italia na kiungo huyo ni nguzo muhimu katika safari hiyo, akiwa amechangia mabao manane katika mashindano yote msimu huu.

"Pogba ni mchezaji wa Juventus na bado anaendelea na mkataba na sisi… Yeye pia alituambia kuhusu nia yake ya kubaki na sisi. Masharti yote yapo kwa ajili yake kuendelea na Juventus kwa miaka ijayo," alisema Marotta ingawa amekiri kuwa katika soka lolote linaweza kutokea.


Comments