DAVID DE GEA anajiandaa kubaki Manchester United kufuatia ripoti kwamba Jose Mourinho atachukua mikoba ya ukocha Old Trafford.
Kipa huyo alibakisha hatua chache tu kuachana na United na kwenda Real Madrid kiangazi kilichopita, na wakati uvumi wa sasa ukianza kushika kasi, ameripotiwa kuvutiwa na mazungumzo kwamba Mourinho anakwenda Old Trafford.
Gazeti maarufu la Hispania, El Pais limedai wikiendi iliyopita kuwa mazungumzo yamefikiwa, huku Bleacher Report likiripoti kwamba De Gea atabaki kama Mourinho atawasili United.
Hata hivyo, inaelezwa kwamba kama Louis van Gaal ataendelea kubaki United, kuna uwezekano wa kipa huyo kuondoka, lakini vinginevyo dili kwa Special One linatarajiwa kubadili mchezo.
Comments
Post a Comment