JOHAN CRUYFF KUPEWA UWANJA UHOLANZI


JOHAN CRUYFF KUPEWA UWANJA UHOLANZI

Johan Cruyff

Shirikisho la soka la nchini Uholanzi wanajiandaa kumpa heshima ya aina yake hayati Johan Cruyff kwa kuupa jina jipya uwanja wa soka Amsterdam Arena. Uwanja huo ulijengwa mwaka 1996 ukitumika kama uwanja wa nyumbani wa timu ya Ajax ambayo Cruyff alicheza enzi za utoto wake.

Nyota huyo wa soka la kisasa alifariki Alhamisi March 24 mwaka huu akiwa na umri wa miaka 68.

Rais wa KNVB Michael van Praag amehuzunishwa na kifo cha Cruyff lakini akafurahishwa na maisha yake: Nasubiri kwa hamu tutakapokuwa tunaupa uwanja wetu jina jipya la Johan Cruyff Arena. Ni heshima kubwa ambayo tunaweza kumpa.

Johan Cruyff

Feyenoord walisimamisha mchezo wao dhidi ya Sparta Rotterdam dakika ya 14 kumpa heshimba Cruyff wakikumbuka namba 14 kama namba bora katika historia ya soka.

Kitendo hicho kilifanyika tena kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya Uholanzi dhidi ya Ufansa jana usiku ambapo Ufaransa ilishinda kwa bao 3-2.



Comments