Joe Hart na Raheem Sterling watakosa mechi za kirafiki za England dhidi ya Germany na Holland baada ya nyota hao wawili wa Manchester Citykuumia na kutolewa katika mchezo wao na Manchester United.
Kipa huyo wa Manchester City aliumia mguu wake wa kulia katika harakati za kumuwahi Anthony Martial asifunge baada ya pasi mbovu ya nyuma kutoka kwa beki Martin Demichelis.
Sterling alitolewa kipindi cha kwanza baada ya kugongana na Juan Mata.
Kipa wa Manchester City Joe Hart katika tukio lililomletea majanga
Raheem Sterling akigaragara chini
Hart akiongea na Gael Clichy baada ya kuumia mguu
Sterling aliumia baada ya kuvaana na Juan Mata
England No 1 Hart akitolewa dimbani kwa macheza
Kwa mujibu wa kocha wa City, Manuel Pellegrini nyota hao watakuwa nje kwa mwezi mmoja na kutia doa maandalizi wa Timu ya Taifa kwaajili ya Euro 2016, ambapo England itajipima nguvu na Ujerumani huko Berlin Jumamosi ijayo kabla ya kurejea Wembley kuikabili Holland siku tatu baadae.
Comments
Post a Comment