MCHEZAJI wa zamani Liverpool, Jamie Carragher, amesema Luis Suarez amemsaidia kwa kiasi kikubwa staa mwenzake katika kikosi cha Barcelona, Lionel Messi kurudi tena kuwa mchezaji bora wa dunia na kwamba anaweza hata kuwa No. 1 yeye mwenyewe.
Carragher na Suarez walicheza pamoja Liverpool misimu miwili na nusu, kabla beki huyo wa muda mrefu kustaafu mwisho wa msimu wa 2012-13, na mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uruguay kuhamia Barcelona kwa dau la euro milioni 80 kiangazi kilichofuata.
Akizungumza katika mahojiano na gazeti la AS, Carragher alisema kwamba Suarez mwenye miaka 19, alimsaidia Messi kuchukua tena nafasi yake kama mchezaji bora wa dunia kutoka kwa Cristiano Ronaldo, na hata ana uwezekano wa kuwa bora kuliko masupastaa wote hao wawili.
"Suarez anasisimua, ni mshambuliaji bora wa kati duniani," alisema Carragher. "Ni miongoni mwa wachezaji watatu wa juu, pamoja na Messi naRonaldo. Amechangia moja kwa moja kuifanya Barca hii kuwa bora zaidi kuliko iliyosimamiwa na (Pep) Guardiola.
"Nilidhani hili halitawezekana,lakini yeye amesaidia kumfanya Messi kuwa bora tena duniani. Changamoto sasa, nikwa ajili yake (Suarez) kuwa No 1, na naamini anakipaji cha kufanya hivyo. "
Comments
Post a Comment