HIVI NDIVYO KAZIMOTO ALIVYOONESHA FURAHA YAKE BAADA YA STARS KUIFUNGA CHAD


HIVI NDIVYO KAZIMOTO ALIVYOONESHA FURAHA YAKE BAADA YA STARS KUIFUNGA CHAD

Nahodha wa Stars Mbwana Samatta akipiga story na nyota              mwenzake waliyewahi kucheza pamoja Simba kabla ya Samatta              kwenda TP Mazembe na Kazimoto kwenda uarabuni

Wakati mwingine ushindi huwa mtamu na kujikuta unafurahi na kufanya vitu vingi ili kuonesha furaha yako kutokana na ushindi ulioupata katika jambo husika.

Kiungo wa wekundu wa Msimbazi na timu ya taifa ya Tanzania Mwinyi Kazimoto, yeye furaha yake ya ushindi ameionesha kwenye kupitia account yake ya facebook mbapo ameanfika ujumbe wenye kauli ya Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda ambayo kuna wakati aliitumia Bungeni na kauli hiyo ikapata umaarufu mkubwa sana 'wapigwe'.

Hii hapa ndiyo kauli ambayo imeandikwa na mchezaji huyo mzoefu kwenye soka la Bongo na kimataifa pia.

"Hakuna namna zaidi ya kupigwa,,,,watanzania wamesema wachad wapigwe na wamepigwa hakuna namna,,,,‪#‎TANZANIA kwanza…", hivyo ndivyo ujumbe huo wa Kazimoto unavyosomeka.

Kazimoto alikuwa miongoni mwa wachezaji wa Stars walioanza kwenye kikosi cha kwanza na baadaye akapumzishwa na nafasi yake ikachukuli John Bocco 'Adebayor'.



Comments