Jaji wa mahakama yaa huko Rio de Janeiro leo Ijumaa amekamilisha kesi na Neymar amekutwa na kosa la kukwepa kodi kwenye vitu vitatu ambavyo ni mkataba wake na Barcelona,Nike na Santos.
Kwenye hukumu hiyo ametakiwa kulipa €45.9m (karibia Tsh 11,305,648,576) kama faini na kodi ambazo alizozikwepa. Kutokana na mashtaka hayo Neymar inasemekana alikwepa kodi baada kwa kutumia kampuni zake Neymar Sport e Marketing, N & N Consultoria na N & N Administracao de Bens kukwepa kodi kati ya mwaka 2012 hadi 2014.
Kampuni ya kukagua mahesabu ambayo ilipewa kazi na mahakama kukagua vitabu vya biashara vya kampuni hizo imesema, "Tumepitia information zote kutokana na kesi hii inavyojieleza juu ya kampuni tatu za Neymar. Kwenye hizo kampuni tatu tumegunfua kwamba kuna vitu vimefanyika kwenye kibiashara kinyume na utaratibu na kukwepa kodi ya serikali".
Pia Neymar bado anafanyikwa uchunguzi huko Spain kwa kosa linalofanana na hili. Mwaka 2013 ambavyo alivyokua ana hamia Barcelona kutoka Santos inasemekana kulifanyika swala la ukwepaji kodi. Lakini kwa sheria za Brazil bado Neymar ana nafasi ya kukata rufaa kama alivyofanya kutokana na maamuzi yaliyopita.
Comments
Post a Comment