GONZALO HIGUAIN ARIPOTIWA KUJIUNGA NA MANCHESTER UNITED KWA MSIMU UJAO ...hiyo ni kazi ya Jose Mounrinho
FOWADI wa Napoli, Gonzalo Higuain ameripotiwa kukubali dili la kujiunga na Manchester United kiangazi hiki baada ya wakala wake kukutana kwa siri na Jose Mourinho.
Kwa mujibu wa mwandishi Mtaliano, Emanuele Giulianelli, kocha huyo raia wa Ureno alikutana na wakala huyo, Nicolas ambaye pia ni kaka wa Higuain mapema wiki hii na dili la miaka mitano lenye thamani ya pauni milioni 7.5 kwa kila mwaka lilikubaliwa.
Mourinho anatarajiwa kutua Old Trafford kiangazi hiki kama Louis van Gaal atatupiwa virago na katika kipindi hiki cha kuelekea usajili, United inaonekana kupita katika njia iliyopita wakati wa kutua David Moyes ambapo tayari klabu hiyo ilikuwa na madili mezani kwa ajili ya Ander Herrera na Luke Shaw.
Higuain amekuwa katika kiwango kizuri msimu huu, akifunga mabao 29 katika mechi 38 alizocheza hadi sasa, rekodi iliyomsukuma Mourinho kutaka kwenda naye Old Trafford ambako ana wasiwasi na safu ya ushambuliaji iliyo chini ya Van Gaal kukosa makali.
Comments
Post a Comment