GERARD PIQUE AWAVULIA KOFIA CRISTIANO RONALDO, ROBERT LEWANDOWSKI NA DIDIER DROGBA



GERARD PIQUE AWAVULIA KOFIA CRISTIANO RONALDO, ROBERT LEWANDOWSKI NA DIDIER DROGBA
Spanish newspaper            Sport claims Gerard Pique has been fined €6,200 for being late            at Barcelona

BEKI staa wa Barcelona na Hispania, Gerard Pique amewataja Cristiano Ronaldo, Robert Lewandowski na Didier Drogba kuwa mastraika watatu ambao hatawasahau kwa "shughuli" waliyompa alipokutana nao dimbani kwa vipindi tofauti.

Akizungumza katika video iliyowekwa katika mtandao wa AS, beki huyo wa kati mwenye umri wa miaka 29, amekiri kuwa washambuliaji hao watatu ndio waliomsumbua zaidi katika maisha yake ya soka.

Alisema: "Mmoja kati yao alikuwa Drogba – mmoja wa mastraika bora niliopata kuwaona. Alikuwa na kila kitu. Kasi, nguvu, mzuri hewani – alikuwa wa ajabu.

"Mwingine alikuwa Cristiano Ronaldo. Nilikutana naye mara kibao na ni mmoja wa wachezaji bora katika historia. Hakika amekamilika, anajua jinsi ya kufunga, kusaidia, kupiga free-kicks, penalti. Yeye anaweza kufanya kila kitu.


    "Lewandowski ni mwingine. Ni mrefu, anaweza kutumia miguu yote. Hakika ni vigumu kumchunga mchezaji wa aina hii. Huwezi kujua nini atafanya."


Comments