Kocha Gary Neville amefukuzwa Valencia huku mechi nane zikiwa zimesalia kabla msimu haujamalizika.
Msaidizi wa zamani wa Rafa Benitez enzi za Liverpool Pako Ayestaran, ambaye Neville alimteua kama msaidizi wake mwezi Januari, amechaguliwa kuwa kocha wa muda hadi mwisho mwa msimu.
Mdogo wake na Gary Neville, Phil Neville anatarajiwa kubakia klabuni kama msaidizi wa Ayesteran.
Gary Neville alitegemewa kudumu hadi mwishoni mwa msimu lakini mmiliki wa timu Peter Lim amekuwa kwenye shinikizo lililomlazimisha kuharakisha maamuzi yake baada ya timu kuelea nafasi ya sita kutoka mstari wa kushuka daraja.
Gary Neville ambaye ni beki wa zamani wa Manchester United ametimuliwa Valencia
Neville (kulia) amekuwa kocha wa Valencia tangu mwezi December sambamba na mdogo wake Phil (kushoto)
Comments
Post a Comment