FAHAMU MACHACHE KUTOKA KWA MTANZANIA ANAYECHEZA SOKA ENGLAND



FAHAMU MACHACHE KUTOKA KWA MTANZANIA ANAYECHEZA SOKA ENGLAND
MKchezaji wa Tanzania Adi Yusuf anayecheza Mansfield              Town inayoshiriki ligi daraja la pili England akimiliki              mpira wakati wa mazoezi
MKchezaji wa Tanzania Adi Yusuf anayecheza Mansfield Town inayoshiriki ligi daraja la pili England akimiliki mpira wakati wa mazoezi

Inawezekana Tanzania ikawa na hazina ya wachezaji wengi wanaocheza soka nje ya nchi ambao kama wakitumiwa vizuri wanaweza kulisaidia taifa kupiga hatua mbele zaidi ya hapa tulipo, lakini kutokana na kutokuwa makini kufatilia ni wapi walipo wachezaji hao na maendeleo yao ili kuwajumuisha kwenye kikosi cha taifa.

Adi Yussuf ni mtanzania anayecheza soka nchini England ambaye amejumuishwa kwenye kikosi cha Stars kwa ajili ya mchezo wa kufuzu fainali za mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2017 nchini Gabon. Licha ya kucheza soka huko kwa muda mrefu mechelewa kuitumikia timu ya taifa ambayo inahitaji wachezaji wenye uzoefu mkubwa na wanaokutana na changamoto mbalimbali kutoka kwenye ligi bora.

www.shaffihdauda.co.tz imefanya mahojiano mafupi na Adi Yussuf kuhusu mambo kadhaa yanayohusu maisha yake ya soka, ungana nami hapa ujue kwa ufupi kuhusu Adi Yussuf.

www.shaffihdauda.co.tz: Hii ni mara yako ya kwanza kujiunga na timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', ilikuwaje hadi ukaitwa kwasababu ni muda mrefu unacheza soka Ulaya lakini ulikuwa hauitwi kwenye timu ya taifa?

Adi Yussuf: Nafikiri kwasababu nilifunga goli halafu scout wa Tanzania anayeishi Uingereza lakini anafanya kazi na TFF akanipigia simu akasema timu ya taifa wanakutaka wakanipigia simu nizungumze nao, nimefurahi kuja kwenye timu ya taifa.

www.shaffihdauda.co.tz: Kunakipindi uliwahi kuitwa lakini ikasemekana kwamba timu yako ilikuwekea ngumu kuja kujiunga na timu ya taifa, taarifa hizi zinaukweli wowote?

Adi Yussuf: Ni kweli, kwasababu timu yangu ilikuwa inaelekea kupanda daraja wakasema natakiwa kubaki, nikashindwa kuja.

www.shaffihdauda.co.tz: Unayaonaje mazingira ya Tanzania kiuchezaji kwa muda ambao umekuwa hapa pamoja na wachezaji ambao umekutana nao kwenye timu ya taifa.

Adi Yussuf: Wachezaji wote ni wazuri na kiloa kitu kipo vizuri na style ya mpira pia ni nzuri.

www.shaffihdauda.co.tz: Watanzania wangependa kujua unacheza timu gani huko England

Adi Yussuf: Timu ninayocheza inaitwa Mansfield Town ipo daraja la pili tupo nafasi ya saba kwahiyo tunaweza tukapanda hadi daraja kwanza.

www.shaffihdauda.co.tz: Kabla ya kwenda England, umetokea wapi na ulikuwa unacheza timu gani?

Adi Yussuf: Nimezaliwa Zanzibar lakini baba yangu alikuwa anacheza Coastal Union, kwahiyo nimeishi sana Tanga kwasababu mama yangu amezaliwa pale na walikuwa wanaishi huko kwa muda mrefu.

www.shaffihdauda.co.tz: Nini matarajio yako kuelekea mchezo wa marudiano siku ya Jumatatu dhidi ya Chad?

Adi Yussuf: Lazima tushinde mchezo wa Jumatatu na endapo nikipata nafasi lazima ntafunga.

www.shaffihdauda.co.tz: Unafikiri kuna siku utarudi Tanzania na kucheza ligi ya hapa?

Adi Yussuf: Nina ndoto siku moja nirudi Tanzania na kucheza soka hapa. Kwasababu mara nyingi babayangu amekua akinisimulia kuhusu soka Tanzania hasa Coastal Union na mimi nimekuwa mfuatiliaji mzuri wa Coastal kwasababu ni timu ambayo babayangu alicheza.



Comments