Baada ya mwimbaji wa Double M Plus Dogo Rama kuonekana kwenye jukwaa la bendi ya kupita iliyojulikana kama Amani Kwanza, msanii huyo ametamba kuwa yeye ni mchezaji wa kulipwa.
Dogo Rama alipanda jukwaa hilo la Amani Kwanza Band Ijumaa iliyopita ndani ya Mango Garden ambapo Saluti5 ilipomuuliza kulikoni, alisema yeye ni kama Messi hivyo lazima awe kimbilio la wengi.
Kama vile hiyo haitoshi, Dogo Rama ameweka picha kwenye ukurasa wake wa facebookiliyomuonyesha akiwa kwenye jukwaa la Amani Band na kuandika kuwa yeye ni mchezaji wa kulipwa.
Katika picha hiyo iliyokuwa imepigwa na Saluti5, Dogo Rama akaisindikiza na maneno yaliyosema: "Mchezaji wa kulipwa, fungua pochi twende sawa."
Hiki ndicho alichoandika Dogo Rama
Comments
Post a Comment