DAVID BECKHAM alitundika daluga miaka mitatu iliyopita, lakini bado mwanasoka huyo anaingiza pesa nyingi ile mbaya.
Nahodha huyo wa zamani wa England anashika nafasi ya pili kati ya wanamichezo wastaafu wanaoingiza mamilioni ya pesa ambapo kwa mujibu wa jarida la Forbes, Beckham ameingiza pauni milioni 45 mwaka 2015.
Mchezaji wa zamani wa mpira wa kikapu Michael Jordan, aliyeingiza pauni milioni£69 ndiye mtu pekee aliyemzidi Beckham nyota wa zamani wa Manchester United, Real Madrid, AC Milan na PSG.
Michael Jordan aliyestaafu mwaka 2003 ndiye mwanamichezo mstaafu anayeingiza pesa miongoni mwa wanamichezo wastaafu duniani. Hiyo inaonyesha kwamba katika wanasoka wastaafu, Beckham ndiye kijogoo wao.
Comments
Post a Comment