Supastaa wa zamani wa Manchester United David Beckham ameonyesha kukunwa na kinda wa klabu hiyo Marcus Rashford.
Beckham amefurahishwa na namna kijana huyo wa miaka 18 alivyofunga bao pekee dhidi ya mahasimu wao Manchester City, lakini kubwa zaidi alivutiwa na ushangiliaji wake uliojaa hisia zilioonyesha jinsi alivyo na mapenzi kwa klabu.
Katika mchezo huo uliochezwa Jumapili kwenye dimba la Etihad, Rashford akafunga kwa umakini mkubwa dakika ya 16, bao lililodumu hadi mwisho wa mchezo.
Ushindi huo umeweka hai matumaini ya Manchester United kumaliza katika nafasi ya nne na kupata tiketi ya kucheza Ligu ya Mabingwa msimu ujao.
Beckham akatupia picha ya kinda huyo kwenye ukurasa wake wa Instagram sambamba na sentesi tamu ya kumsifia.
Marcus Rashford amemkuna Beckham
Comments
Post a Comment