CHELSEA YATENGA PAUNI MIL 31 KUMNASA BEKI KOSTAS MANOLAS WA ROMA


CHELSEA YATENGA PAUNI MIL 31 KUMNASA BEKI KOSTAS MANOLAS WA ROMA

CHELSEA ipo tayari kupeleka ofa ya uhamisho kwa beki wa kimataifa wa Ugiriki anayekipiga katika klabu ya AS Roma ya Italia, Kostas Manolas.

Manolas amecheza mechi 57 akiwa na Roma tangu ajiunge na timu hiyo ya Serie A kutoka Olympiacos ya Ugiriki mwaka 2014, lakini sasa anahusishwa na kuhamia katika Premier League.

Gazeti la Il Tempo limesema kuwa Chelsea inajiandaa kumpeleka Stamford Bridge beki huyo mwenye umri wa miaka 24 kwa dau la pauni milioni 31.4 mwishoni mwa msimu.

Hata hivyo, Roma chini ya Luciano Spalletti inataka kumbakisha Manolas licha ya klabu kubwa barani Ulaya kupigana vikumbo kumuwania ikiwamo pia Arsenal.


Comments