CHELSEA YATAKIWA KUONGEZA DAU ILI KUMNASA BEKI KOSTAS MANOLAS ATAKAYEKUWA MRITHI WA JONH TERRY




CHELSEA YATAKIWA KUONGEZA DAU ILI KUMNASA BEKI KOSTAS MANOLAS ATAKAYEKUWA MRITHI WA JONH TERRY
Signing: Roma paid            Olympiacos ¿13m (£10.35) for the services of Greek  defender            Kostas Manolas

CHELSEA ilifeli dili lake kwa Kostas Manolas wa AS Roma inayemtaka kwa ajili ya kumrithi nahodha wao John Terry, lakini sasa itaweza kufanikisha uhamisho wa beki huyo kama itakuwa tayari kulipa pauni milioni 35.

Roma iko tayari kufanya biashara kwa beki huyo raia wa Ugiriki, ambaye pia anafukuziwa na Arsenal.

Kwa mujibu wa The Sun, Chelsea inapaswa kupanda dau kama ina nia ya dhati ya kumpeleka Manolas Stamford Bridge, baada ya ofa yao ya kwanza ya pauni milioni 26 kukataliwa.

Kiwango cha Manolas katika Serie A kimeikuna Chelsea na ripoti zinaeleza kuwa klabu hiyo inafuatilia kwa karibu kuweza kufanikisha dili la beki huyo wa kati mwenye umri wa miaka 24.


Comments