CHELSEA INA LAKE JAMBO KWA KIUNGO N’GOLO KANTE WA LEICESTER CITY



CHELSEA INA LAKE JAMBO KWA KIUNGO N'GOLO KANTE WA LEICESTER CITY

CHELSEA inapanga kumfanya kiungo wa Leicester City anaekuja juu kwa kasi, N'Golo Kante, kuwa usajili wake wa kwanza kiangazi hiki.

Kante amekuwa 'injini' ya Leicester katika safari yake ya kushtua iliyowaweka kileleni mwa Premier League msimu huu, wakati Chelsea ikihangaika katikati ya msimamo wa ligi hiyo.

Kwa mujibu wa Daily Mirror, the Blues inaweza kumfanya Kante kuwa usajili wake namba moja katika zama mpya za Antonio Conte, akifananishwa uwezo wake na gwiji aliyetamba Chelsea miaka hiyo, Claude Makelele.


Hata hivyo, Conte anaweza kuwa na malengo yake kichwani kuhusu uhamisho, baada ya Chelsea kuhusishwa na viungo wenye majina makubwa katika siku za karibuni kama Arturo Vidal na Radja Nainggolan.


Comments