BMM BAND WAKO JM HOTEL MANZESE LEO USIKU



BMM BAND WAKO JM HOTEL MANZESE LEO USIKU

Band mpya ya BMM inayoongozwa na wakali wawili Mule Mule na Totoo ze Bingwa, Jumapili ya leo itajitupa ndani ya ukumbi wa JM Hotel Manzese Tip Top.

BMM Band itakuwa hapo ikiwa ni maalum kwaajili ya kusherehekea sikukuu ya Pasaka huku moja ya ngoma zao inayotarajiwa kutikisa hapo ni "Watabiri".

Bendi hiyo iliyozinduliwa mwezi uliopita ndani ya Mzalendo Pub, inapelekwa JM Hotel kwa hisani ya kampuni ya Boy George Promotion.


Comments