BECKENBAUER AMWAMBIA GUARDIOLA ASAHAU KABISA MPANGO WA KUONDOKA NA WACHEZAJI WA BAYERN MUNICH



BECKENBAUER AMWAMBIA GUARDIOLA ASAHAU KABISA MPANGO WA KUONDOKA NA WACHEZAJI WA BAYERN MUNICH
Douglas Costa has            labelled soon-to-be Manchester City manager Pep Guardiola            'exceptional'

RAIS wa heshima wa Bayern Munich, Franz Beckenbauer amemuonya Pep Guardiola, kwamba litakuwa ni jambo lisilokubalika kujaribu kuchukua mchezaji yeyote katika kikosi chake cha sasa na kumpeleka Manchester City kiangazi hiki.

Guardiola amekubali mkataba wa miaka mitatu City, utakaoanza wakati dili lake Bayern litakapomalizika mwisho wa msimu, na kumekuwa na uvumi kwamba ana nia ya kuondoka na wachezaji kama Manuel Neuer na David Alaba.

Gazeti la Bild liliripoti mwanzoni mwa wiki kwamba kulikuwa na jaribio lililofeli la kumshawishi Alaba kujiunga na City, lakini Mtendaji Mkuu wa Bayern, Karl-Heinz Rummenigge haraka alikanusha stori hiyo, na Guardiola mwenyewe huko nyuma alipata kusema kuwa ana nia ya 'kuiba' mchezaji yeyote Allianz Arena.

Beckenbauer, ambaye alipata mafanikio makubwa akiwa mchezaji wa Bayern na baadaye kuwa kocha katika vipindi viwili tofauti kabla kuwa rais wa klabu, alisema hatarajii Guardiola kushawishi mchezaji yeyote kumfuata, lakini akamuonya dhidi ya jitihada zozote za kufanya hivyo.


"Hii haiwezi kutokea," alisema Beckenbauer kuliambia gazeti la Bild. "Kama ni kweli, hii haikubaliki, lakini sidhani kama Guardiola ana uwezo wa kufanya hivyo."


Comments