BAADA YA KUPEWA KIGINGI CHA DORTMUND, KLOPP ANENA JAMBO.


BAADA YA KUPEWA KIGINGI CHA DORTMUND, KLOPP ANENA JAMBO.
Klopp Enzi akiwa na klabu ya Dortmund
Klopp Enzi akiwa na klabu ya Dortmund

Jurgen Klopp anena ' dunia lazima itatulia kutizama ' Liverpool ikipambana na Dortmund. Jurgen Klopp ameenda mbali zaidi na kusema mpambano wa  Europa League kati ya Liverpool dhidi ya Borussia Dortmund ni " hadithi ambayo soka pekee ndilo linaloweza kuiandika "  "Kiukweli nimefurahishwa na droo hii iliyofanyika ," Klopp aliiambia tovuti rasmi ya klabu ya Liverpool.

"Kwa nini upende kukutana na klabu bora na imara zaidi kwenye mashindano? Lakini, ni wazi kama unataka kushinda Europa League basi unatakiwa kuzifunga timu zenye nguvu . "Ni bora sana kucheza dhidi yao katika mechi mbili kuliko katika mchezo mmoja tu , nami ni kweli na furaha na nitawaonyesha vijana wangu namna ulivyo uwanja huu wa ajabu na mji wa kipekee. Hii  ni hadithi ambayo soka pekee ndilo linaloweza kuiandika."

Liverpool imevuka kuelekea hatua inayofuata baada ya kuwachapa wapinzani wao wa jadi, Manchester United kwa ujumla wa michezo miwili na kufanikiwa  kufikia hatua ya nane bora na ujira ambao pengine Klopp atakuwa kaupata, ni ujio wa ratiba hii iliyotoka ambayo yeye binafasi anaamini ni kuelekea kuikamata dunia ya soka katika mchezo huu.

"Viwili kati ya klabu vikubwa zaidi duniani kukutana katika Europa League, hivyo kila mtu ambaye pengine alidhani miezi michache iliyopita labda haya hayakuwa mashindano ya kuvutia, kwa sasa nina imani wameweza kubadili mlengo wa kifikra na akili zao katika wiki chache zilizopita , "Klopp aliongeza.

"Michezo dhidi ya Manchester United uliwakutanisha wakubwa wawili, na sasa unafuata moja kati ya michezo mikubwa kupindukia dhidi ya Dortmund. Kwenda Dortmund na kucheza katika uwanja Dortmund (Signal Iduna Park) ni moja ya mambo bora unayoweza kufanya katika soka.

"Wana kikosi kizuri na  ni wapinzani wenye nguvu sana, lakini sisi sio wabaya pia! Kila mtu anajua michezo yetu bora tumeicheza dhidi ya timu bora. Ni wazi na ni michezo miwili ambayo nadhani dunia nzima itatakiwa kuangalia ."

Lakini Klopp ameweka bayana kuwa anachukia tu jambo moja juu ya mchezo huu kuwa pindi utakapokaribia atatizamwa sana na kuwekwa karibu kwa kila jambo kutokana na historia yake na klabu hiyo pia mahusiano yake ya karibu yaliyokuwepo baina yake na klabu hiyo aliyoisaidia kushinda mataji mawili ya Bundesliga 2011 na 2012.

 



Comments