Gary Neville aliacha kazi ya kuwa mchambuzi wa soka na kwenda kuwa kocha kwenye club ya Valencia kwenye ligi ya Hispania. Akiwa na club hiyo ameshindwa kuisaidia na kufikia hatua ya kufukuzwa kazi ndani ya miezi 4 tu.
Akiwa ndani ya Valencia, Neville ameweza kupata ushindi mara 3 tu kwenye mechi 16 za ligi. Pia aliwahi kupata aibu ya kufungwa 7-0 kutoka kwa Barcelona kwenye mchezo wa nusu fainali ya Copa del Rey kwenye mchezo wa kwanza mwezi February.
Pako Ayestaran atakua kocha wa club hiyo hadi mwisho wa msimu huu akiwa ana saidiana na Phil Neville ambae bado atabaki.
Sky Sports wamesema kwamba mlango upo wazi kwa Gary Neville kurudi kuwa mchambuzi wa soka kama zamani kama atahitaji kurudi. Kabla hajaenda kuwa kocha wa Valencia Neville alikua anachambua soka kwenye kituo cha television cha Sky Sports.
Mchezaji wa Real Madrid ameonesha kumpa-support Gary Neville kwa kusema kwamba angepewa muda zaidi angeweza kuonesha jinsi gani anajua soka. Ni aibu kuona kwamba amefukuzwa kazi.
Valencia ipo nafasi ya 14 ikiwa na pointi 34 baada ya kucheza mechi 30, kati ya mechi hizo Valencia imeshinda mechi 8, sare 10 huku iliwa imepoteza michezo 12.
Comments
Post a Comment