ARSENE WENGER KUONDOKA ARSENAL IWAPO …


ARSENE WENGER KUONDOKA ARSENAL IWAPO …

BODI ya Klabu ya Arsenal bado ipo nyuma ya Arsene Wenger, lakini kama mashabiki wataendelea kumshinikiza aondoke kutokana na timu kuelekea kukosa taji kwa mara nyingine, hatakuwa na chaguo zaidi ya kufunga virago mwisho wa msimu.

 Kutokana na kuongezeka presha baada ya Arsenal kupoteza mechi ya FA Cup dhidi ya Watford Jumapili iliyopita, magazeti ya Daily Mirror na Daily Telegraph yameripoti kuwa Wenger ataachwa na bodi ya klabu kuamua mustakabali wake wakati akielekea kuingia mwaka wake wa mwisho wa mkataba msimu ujao.

Lakini vyanzo vya karibu na Wenger, vimepasha kuwa Mfaransa huyo ataamua kubwaga manyanga kama 'hali ya hewa' itazidi kuwa mbaya Emirates katika hatua ya mwisho ya msimu kiasi cha kuanza kuathiri timu.


Tayari kuna tetesi kwamba Arsenal inawatazama Diego Simeone na Manuel Pellegrini kama mbadala wa Wenger mwenye umri wa miaka 66, aliyedumu na timu hiyo tangu mwaka 1996 na kuandika rekodi ya kuwa kocha aliyehudumu muda mrefu kuliko wote waliopita.


Comments