ARSENAL YAMNYATIA JORGINHO WA NAPOLI



ARSENAL YAMNYATIA JORGINHO WA NAPOLI

JOAO SANTOS, wakala wa kiungo wa Napoli ya Italia, Jorginho amethibitisha kwamba klabu ya Arsenal imevutiwa na mteja wake.

Kiungo huyo mzaliwa wa Brazil mwenye uraia wa Italia, amekuwa midomoni mwa wapenda soka walio wengi baada ya kung'ara kwenye kiungo cha Napoli, akiisaidia kuwa mshindani wa ukweli katika mbio za ubingwa wa Serie A msimu huu.

Kiwango cha staa huyo anayemudu zaidimwenye umri wa miaka 24 pia kinaonekana kuwa ushawishi kwa kocha wa Italia, Antonio Conte kumjumuisha kwenye kikosi cha Euro 2016.

Mbali ya Arsenal na Conte, kiungo huyo pia amezitamanisha klabu nyingine kubwa, ikiwamo Real Madrid ambayo ilimpelekea salamu za pongezi baada ya kufanya mambo makubwa dhidi ya Palermo.

Jorginho anayecheza kama kiungo wa ulinzi, huku akimudu pia nafasi ya kiungo mchezeshaji, anaonekana kuwa na uwezo wa 'kufiti' katika staili ya Arsenal ya kupiga pasi.



Comments