ARSENAL inataka kumsainisha kiungo wa Reading anayekipiga pia katika kikosi cha England cha vijana wa umri chini ya miaka 20, Aaron Kuhl kwa mkataba huru mwisho wa msimu huu.
Kuhl mwenye umri wa miaka 20, ambaye mwaka jana alihusishwa na mipango ya kwenda Manchester City, ni mchezaji mwenye kipaji anayetamba na klabu hiyo inayoshiriki Ligi ya Championship – Daraja la Kwanza nchini England.
Dili lake kwenda City lilishindikana, lakini mtandao wa Transfermarketweb umeripoti kuwa anaweza kujiunga na klabu kubwa ya Premier League mapema iwezekanavyo, huku Arsenal ikionekana kuvutiwa naye.
Kiungo huyo wa ulinzi aliye hodari kwenye kusambaza pasi, anatakiwa pia na West Ham.
Comments
Post a Comment