ANTHONY MARTIAL ASEMA ANAJIFUNZA KUPITIA KWA CRISTIANO RONALDO



ANTHONY MARTIAL ASEMA ANAJIFUNZA KUPITIA KWA CRISTIANO RONALDO
Manchester United            youngster Anthony Martial is all smiles during a Manchester            United training session
STRAIKA wa Manchester United, Anthony Martial amefichua kwamba anajaribu kujifunza kutoka kwa staa wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo.

Martial alianza maisha Old Trafford kwa kishindo akithibitisha alistahili uhamisho wa siku ya mwisho kwa pauni milioni 38 kutoka Monaco, akifunga dhidi ya mahasimu wao wakubwa Liverpool katika mechi yake ya kwanza.

Baada ya kuona ushujaa wake wa kupiga mabao ukipungua kasi katika wiki za hivi karibuni, Martial alijikuta akitumika pembeni wakati kinda Marcus Rashford akiendelea kuongoza safu ya ushambuliaji.

Alipobaini mazungumzo kuhusu nafasi yake bora dimbani, Martial akabainisha katika mahojiano kabla mechi ya Manchester derby kwamba 'anapenda' kucheza pembeni, lakini anahisi ndani ya nafsi yake kwamba yeye hasa ni straika.

"Mimi ni Straika, lakini napenda kucheza pembeni," alisema Martial katika mahojiano na Sky Sports. "Jambo kubwa ni kuwa popote ninapocheza nafurahia na kusaidia timu."

"Lazima niendelee kujituma zaidi mazoezini. Nahitaji kufikiri zaidi kama mfungaji, wakati mwingine nazama zaidi katika mchezo kwa sababu napenda sana uchezaji wa jumla.


"Mtu kama Cristiano Ronaldo analenga kuendelea kufunga, na pengine na mimi nahitaji kufikiri zaidi kuhusu kufunga."


Comments