ZINEDINE ZIDANE ASEMA YEYE NI SHABIKI WA LEICESTER CITY


ZINEDINE ZIDANE ASEMA YEYE NI SHABIKI WA LEICESTER CITY

ZINEDINE ZIDANE ameweka wazi kuwa yeye ni shabiki wa Leicester City na kusema kuwa itakuwa jambo la kusisimua kuwaona katika Champions League msimu ujao.
Baada ya kunusurika kushuka daraja msimu uliopita, Leicester City wamecharuka msimu huu na sasa wanaongoza msimamo wa Ligi Kuu ya England huku zikiwa zimesalia mechi 12.
Na kwa mujibu wa kocha huyo wa Real Madrid, kiwango cha Leicester City kimeishtua bara zima la Ulaya.
Zidane anasema: "Katika hatua hii ya ligi, Leicester kuwa kileleni ni mafanikio yaliyotukuka.
"Wamekuwa gumzo sio England pekee bali Ulaya nzima. Kukiwa na timu zenye majina makubwa England na pesa za kumwaga, wakifanikiwa kutinga Champions League itakuwa ni jambo la kipekee katika soka."



Comments