WILLIAN AGEUKA LULU CHELSEA, AANDALIWA DILI LA KUBAKI HADI 2020


WILLIAN AGEUKA LULU CHELSEA, AANDALIWA DILI LA KUBAKI HADI 2020
The Brazil            international (centre) has been a standout performer this            season despite the club's struggles

CHELSEA imemuwekea mezani kiungo wake Willian ofa ya mshahara mpya wa pauni 120,000 kwa wiki ili kuweza kumbakisha Stamford Bridge hadi mwaka 2020.

Kwa mujibu wa gazeti la The Times, Chelsea tayari imeanzisha mazungumzo na kiungo huyo Mbrazili mwenye miaka 27 wakitaka kumpa dili la miaka minne litakalomwezesha kuweka kibindoni jumla ya pauni milioni 25.

Chelsea iliyotema pauni milioni 30 kumnunua Willian katika klabu ya Anzhi Makhachkala ya Russia mwaka 2013, imeripotiwa kuwa na presha kwamba kupanda kwa kiwango cha Willian msimu huu, kumezivutia klabu nyingine kubwa barani Ulaya.

Mabingwa wa Ufaransa, Paris Saint-Germain wanaelezwa kuandaa ofa sambamba na miamba ya Ujerumani, Bayern Munich na vinara wa Serie A, Juventus.

The Times limedai kuwa Chelsea ina wasiwasi kwamba inaweza kukosa nafasi ya kucheza Champions League msimu ujao kupitia 'Top Four' ya Premier League, hivyo kuwa kichocheo cha kumkimbiza kiungo huyo aliyebakisha miaka miwili na nusu katika mkataba wake wa sasa.



Comments