Kocha huyo mwenye umri wa miaka 64 aliondoka kwenye uwanja wa Greenhous Meadow Jumatatu usiku na alinaswa na kamera wakati akihojiwa kama kuna chochote ambacho anmaweza kuwaeleza mashabiki wa Man United wakati aliposimamishwa kusaini vitabu vya kumbukumbu.
Akijibu swali hilo, Van Gaal alisema kwa ufupi kwamba bado ataendelea kuinoa klabu hiyo huku akidai kuwa anakwenda kupigania siku nyingine baada ya kuishuhudia timu hiyuo ikiondoka na ushindi huo wa mabao 3-0 katika mchezo wa marudiano na timu hiyo ya Ligi daraja la kwanza.
Mholanzi huyo amekuwa chini ya shinikizo kubwa baada ya kufungwa na timu ya Midtjylland katika michuano ya Ligi ya Europe huku ikiwa imeshafungwa na timu inayotabiriwa na tishio la kushuka daraja ya Sunderland, katika michuano ya Ligi Kuu England wiki moja kabla.
Hata hivyo usiku wa kuamkia jana timu hiyo ikafanikiwa kutinga robo fainali ya m,ichuano hiyo ya Kombe la FA kirahisi na sasa itaivaa Westham ikiwa kwenye uwanja wake wa Old Trafford.
Kwa sasa Man United inashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu England, ikiwa nyuma kwa pointi sita dhidi ya mahasimu wao, Manchester City wanaoshika nafasi ya nne, lakini hata hivyo, Van Gaal amegoma kukata tamaa kama atafuzu kucheza kwenye michuano ya Klabu Bingwa msimu ujao.
"Kila kitu kinawezekana," alisema kocha huyo. "Bado tunashiriki kwenye mashindano matatu kwahiyo tunatakiwa kupigania nafasi zetu zote."
Alisema, tangu mwanzo kila mtu alikuwa akisema kwamba Man United wataondoka na ushindi dhidi ya Shrewsbury na hivyo akasema jambo hilo ni zuri kwa wachezaji kutokana na kuwa kwa sasa wametinga robo fainali ya Kombe la FA.
Comments
Post a Comment