LOUIS VAN GAAL amefichua siri iliyo nyuma ya ushindi wa mabao 3-0 waliopata Manchester United katika mechi ya FA Cup dhidi ya Shrewsbury Jumatatu usiku, akisema kuwa 'waliiba' mbinu ya Midtjylland ya Denmark iliyowachapa 2-1 katika Europa League wiki iliyopita.
Mabao kutoka kwa Chris Smalling, Juan Mata na Jesse Lingard yalimwezesha Van Gaal kupumua wakati akiiwezesha United kufuzu hatua ya robo fainali.
Van Gaal amesema kwa bao la free-kick iliyopigwa na Mata, walikopi staili iliyotumiwa na Midtjylland kusimamisha wachezaji watatu nyuma ya ukuta wa mabeki ili kumchanganya kipa.
"Tulijifunza kwa sababu tulisoma kwa Midtjylland na kuona wanachokifanya katika kupiga free-kick. Tulidhani ilikuwa 'offside' lakini tulipomuuliza refa Mreno katika mechi ya wiki iliyopita alisena 'hapana siyo offside'. Hivyo unaweza kufanya hivyo, na leo (Jumatatu) usiku tumefunga kwa staili hiyo. Hiyo ni nzuri," alisema Van Gaal.
Akizungumzia bao hilo la Matta, kocha wa Shrewsbury, Micky Mellon alisema hakuona utata wowote zaidi ya bao hilo lililofungwa dakika za majeruhi za kipindi cha kwanza kuwaweka jkatika mlima mrefu wa kupanda wamkiwa nyuma kwa mabao 2-0.
Katika hatua nyingine, Van Gaal amesema bado yupo kwa sana Manchester United, kauli inayokuja katika kipindi ambacho kibarua cha kocha huyo kiko mashakani.
Comments
Post a Comment