USHINDI WA MAN CITY UNAVITU 4 VYA KUJIFUNZA KUTOKA KWA PELLEGRINI



USHINDI WA MAN CITY UNAVITU 4 VYA KUJIFUNZA KUTOKA KWA PELLEGRINI

Manuel P

Manchester City imesheweka mguu mmoja ndani ya robo fainali ya Champions League kutokana na ushindi wa bao 3-1 walioupata ugenini dhidi ya Dynamo Kiev ya Ukraine.

Goli mbili za kipindi cha kwanza kutoka kwa Sergio Aguero na David Silva, zinaiweka Man City kwenye nafasi ya kuweka historia kwenye michuano hiyo mikubwa.

Huku bao la tatu la Yaya Toure la sekunde chache kabla ya pambano kumalizika likizidi kupunguza matumaini ya Dynamo na kuwapa nafasi kubwa City kusonga mbele.

Toure-City

City haijawahi kufuzu kucheza robo fainali ya michuano hiyo lakini nyota hao wa Etihad huenda watavunja mwiko huo wiki mbili zijazo.

Kocha wa City Manuel Pellegrini sasa anafuraha kutokana na ushindi huo baada ya kuwapumzisha nyota wake wa kikosi cha kwanza na kushuhudia vijana wake wakichapwa na Chelsea 5-1 kwenye kombe la FA weekend iliyopita.

Lakini tayari mashabiki wamesahahau jambo hilo baada ya kusherekea ushindi wa kihistoria kwenye maisha yao ya Champions League.

city

Dynamo walifuzu hatua ya 16 bora baada ya kuwapa kisago mabingwa wa zamani Porto na kuwarahisishia Chelsea mechi yao ya mwisho ya makundi.

Hata hivyo Dynamo hawajacheza tangu kipindi cha mapumziko cha msimu wa baridi katikati ya mwezi December mwaka uliopita na hiyo inamaanisha vijana wa Sergei Rebrov waliingia kwenye mchezo huo wakiwa hawako kwenye makali yao ya siku zote.

img_3804.jpg

Vitu vinne (4) vya kujifunza

  1. Manuel Pellegrini anawaumbua waliokosoa kuwachezesha wachezaji vijana kwenye mchezo wa FA Cup weekend iliyopita.

Manchester City walipoteza dhidi ya Chelsea lakini walionesha wapya kwenye mchezo dhidi ya Kiev usiku uliopita na kupata magoli ya ugenini kabla ya mchezo wa marudiano pale Etihad Stadium.

Endapo watashinda mchezo wa fainali ya Capital One Cup pale kwenye dimba la Wembley itakuwa ni wiki nzuri kwa boss huyo wa City.

  1. Manchester City hawajawahi kutoboa inapofika hatua ya mtoano wa Champions League.

Msimu uliopita walifuzu hatua ya makundi lakini hawakufika popote lakini usiku uliopita wameamsha matumaini ya kusonga mbelele.

  1. Fernandinho alicheza kama winger wa kulia jana kwenye uwanja wa Olympic.

Mbrazil huyo amezoea kucheza kama kiungo mkabaji lakini kwa mchezo wa jana alipangwa pembeni na alitoa mchango mkubwa kwenye timu.

  1. Bacary Sagna ameonekana kuwa chaguo la kwanza la Manuel Pellegrini kwenye upande wa beki ya kulia kwa sasa.

Hilo ni pigo kubwa kwa mkongwe wa Man City Pablo Zabaleta ambaye angependa kuwepo kwenye kikosi kilichocheza mchezo wa jana.



Comments