ROMAN ABRAMOVICH ATENGA PAUNI MIL 130 ILI KUWANASA ARTURO VIDAL NA JOHN STONES



ROMAN ABRAMOVICH ATENGA PAUNI MIL 130 ILI KUWANASA ARTURO VIDAL NA JOHN STONES
The 28-year-old is            looking forward to facing his former club in the Champions            League on Tuesday night
ROMAN ABRAMOVICH atampatia kocha wake mpya kitita cha pauni milioni 130 kwa ajili ya kusaini masupastaa wanne wakiwamo Arturo Vidal na John Stones ili kukisika upya kikosi cha Chelsea.

Kocha wa timu ya taifa ya Italia - Azzurri, Antonio Conte amechomoza mstari wa mbele wiki hii wakati Chelsea ikisaka kocha wa kudumu kumrithi Jose Mourinho aliyetupiwa virago Desemba mwaka jana na nafasi yake kushikwa kwa muda na Guus Hiddink.

Mkurugenzi wa Ufundi wa Chelsea, Michael Emenalo yuko Italia akichunguza wachezaji na alimtazama staa wa Bayern Munich, Arturo Vidal alipokuwa akicheza dhidi ya Juventus usiku wa Jumanne.

John Stones wa Everton amebaki kuwa lengo kuu katika safu ya ulinzi, licha ya kuwa Chelsea ilifeli jaribio la kumtwaa beki huyo wa kati mwenye thamani ya pauni milioni 40 kiangazi kilichopita.

Mbali ya Conte, makocha wengine walio kwenye listi ya kwenda Chelsea ni Masimillio Allegri wa Juventus, Jorge Sampaoli na Diego Simeone wa Atletico Madrid.


Comments