CHELSEA imemuongeza kiungo Mjerumani wa Real Madrid, Toni Kroos katika listi ya mastaa inaowafukuzia kiangazi hiki, ingawa italazimika kuvunja benki na kulipa pauni milioni 234 ili ikidhi mahitaji ya mkataba wake kwa mujibu wa mtandao wa Football Leaks.
Mtandao wa intaneti wa Calciomercato wa Italia, umedai kuwa Kroos mwenye umri wa miaka 25 ameingia kwenye rada za Chelsea ambayo inahaha kusuka kikosi chake upya baada ya kupoteza mwelekeo msimu huu.
Mmiliki wa Roman Abramovich anapanga kutumia kiasi kikubwa cha fedha kuirudisha klabu yake katika mwelekeo sahihi baada ya kuonekana dhahiri kufeli kutetea taji lake la Premier League msimu huu.
Kroos aliyejiunga na Real Madrid akitokea Bayern Munich mwaka 2014, ana mkataba Bernabeu hadi 2020, lakini Abramovich anaweza kuonyesha 'jeuri ya fedha' na kumng'oa staa huyo.
Comments
Post a Comment